Zaidi ya kuwa tu chakula kinachofaa, asali ni mojawapo ya dawa za zamani zaidi zinazotumika, kwani ina vitamini B nyingi, madini kadhaa, na vitu vyenye uwezo wa kuzuia utendaji wa oksijeni. Dakt. May Berenbaum, mtaalamu wa wadudu katika Chuo Kikuu cha Illinois, Marekani, anasema: “Asali imetumiwa kwa karne nyingi kutibu matatizo mengi ya afya kama vile vidonda, kuungua, watoto wa jicho, vidonda vya ngozi na majeraha ya kukwaruzwa.”
Likieleza kuhusu upendezi wa hivi karibuni kuhusu manufaa za asali kwa afya, Shirika la Habari la CNN linaripoti hivi: “Asali iliacha kupakwa kwenye vidonda wakati dawa za kuua viini vya ugonjwa zilipovumbuliwa wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu. Lakini utafiti mpya na kutokea kwa bakteria zisizoweza kuuawa na dawa hizo umefanya asali ianze kutumiwa tena.” Kwa mfano, sehemu moja ya utafiti huo inahusu kutibu majeraha ya kuungua. Ilionekana kwamba wagonjwa walipona haraka na kuhisi maumivu machache na kuwa na makovu machache walipotibiwa kwa asali.
Uchunguzi unaonyesha kwamba kwa sababu ya kimeng’enya fulani kinachoongezwa kwenye nekta na nyuki, asali ina uwezo wa kupigana na bakteria na viini. Kimeng’enya hicho hutokeza haidrojeni peroksaidi, ambayo huua bakteria hatari. Isitoshe, inapopakwa juu ya kidonda, asali hupunguza mwasho na kuchochea ukuzi wa tishu zinazofaa. Hivyo, mtaalamu wa biolojia na kemia Dakt. Peter Molan wa New Zealand anasema: “Wataalamu wa matibabu wanaiona asali kuwa dawa nzuri, inayofaa kwa matibabu.” Kwa kweli, Shirika la Matibabu la Australia limeidhinisha asali kuwa dawa, na asali huuzwa kama dawa ya kutibu vidonda katika nchi hiyo.
Ni vyakula gani vingine vitamu ambavyo hujenga mwili na vinavyoweza kutumiwa kama dawa? Si ajabu kwamba zamani sheria zilipitishwa ili kulinda nyuki na wafugaji wa nyuki! Ilikuwa kosa kukata miti au kuharibu mizinga yenye nyuki, na mtu angeweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini kubwa au hata kuuawa
This blog is devoted to give out different information concerning honey like different types of honey, their uses, how to differentiate real honey from fake ones and many other things. Come, educate yourself and place your order of good quality honey from honey spring.
Friday, July 12, 2013
MANUFAA YA ASALI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment