Thursday, July 11, 2013

ASALI NI NINI?

Sasa basi Asali ni nini? Asali ni mchanganyiko wa virutubisho mbali mbali, zikiwemo aina ya sukari zinazojulikana kwa jina la Glukosi (Glucose) pamoja na Fruktosi (Fructose), na madini mbalimbali vikiwemo; Magnesium, Copper, Iodine, zinc, Potassium, Calcium, Sodium, Chlorine, Sulfur, Iron na Phosphate, pamoja na vitamin B1, B2, B3, B5, B6, na vitamin C. Vitamin mara nyingi ubadilika kulingana na ubora wa necta, pamoja na chavua. Vile vile kwenye asali, kunapatikana aina mbalimbali za Hormones. Kama inavyoelezwa kuwa asali ni ponyo(kinywaji chenye kutibu) kwa wanadamu, na haya yamethibiti kwa wanadamu hivi leo. Kama ilivyotokea katika mkutano wa wanasayansi,  uliofanyika mwaka 1993 mwezi Sept. tarehe 20-26. Mkutano huu ulifanyika nchini China, na ulijulikana kwa jina la World Apiculture Comference. Na kuchapishwa katika jarida la Horriget News Paper, la tarehe 19th.Oct.1993. Katika mkutano huo matibabu ya kutumia asali yalijadiliwa kwa mapana sana, wanasayansi wa Kimarekani wao walielezea kuwa, ndani ya asali kuna vitu vinaitwa; Royal Jelly, chavua, na ute (Propolis, Bee resin), vitu hivi husaidia sana katika matibabu ya magonjwa mengi. Naye Daktari kutoka Romania, yeye aliwahi kujaribu kutibu mtoto wa jicho (Cataract), kwa wagonjwa 2094, kati yao 2002 walipona kabisa, na hii ni sawa na asilimia 96% ya wagonjwa waliopona kabisa. Daktari huyo alieleza kuwa Bee Resin au ute unaotokana na nyuki, unasaidia kuponyesha magonjwa mengine, mfano magonjwa ya ngozi (Skin Diseases), magonjwa ya kuvuja kwa damu (Haemorrhoid), magonjwa ya uzazi (Gynaecological Diseases) n.k.

No comments:

Post a Comment