Katika vitu ambavyo ni changamoto kubwa sana katika soko la asali na vinawasumbua si tu watumiaji wa asali bali hata wa wauzaji ni kiwango kikubwa cha maji katika asali kuliko kawaida ambacho chanzo huweza kua UWAHISHAJI WA KUVUNA ASALI KABLA HAIJAKOMAA VIZURI au tatizo kubwa zaidi ambalo ni UCHAKACHUAJI WA ASALI KWA KUONGEZA MAJI unaofanywa na wauzaji wasio waaminifu.
Kwa kawaida ASALI YA NYUKI WAKUBWA inakua na kiwango cha maji ya kati ya asilimia 17 mpaka 20 na asilimia inayobaki ni SUKARI. Wakati asali ya nyuki wadogo kiwango cha maji kinakua zaidi ya asilimia 20.
MAJI ni adui mkubwa sana katika asali kwani maji yakizidi hupunguza ubora wa asali, lakini pia huiweka asali katika hatari kubwa ya kuchacha.
Zipo njia nyingi za kienyeji za kupima kiwango cha maji kwenye asali na kujua kama maji yaliyopo ni ya kiwango sahihi ama la! Njia hizo ni pamoja na kutumia MSHUMAA, KARATASI NYEUPE, KUDONDOSHEA ASALI KWENYE KIKOMBE CHA MAJI n.k.
Pamoja na uwepo wa njia hizo lakini honey spring tumekwenda hatua moja mbele na tunatumia kifaa kidogo cha mkononi kinachoitwa REFRACTOMETER ambacho hupima kwa usahihi zaidi kiwango cha MAJI na SUKARI pia katika asali.
Kifaa hichi kinatuwezesha kuingiza sokoni asali ambayo inatakiwa kupelekwa kwa mlaji lakini pia kwa kiwango ambacho mlaji anakitegemea kwenye asali anayonunua!
Kwenye maonyesho ya nane nane(88) mwaka huu mkoani MOROGORO tutakuepo na kuonyesha vizuri zaidi watumiaji jinsi kifaa hichi kinavyofanya kazi.
No comments:
Post a Comment