Wednesday, July 10, 2013

IJUE ASALI ZAIDI

VIRUTUBISHO VILIVYOPO NDANI YA ASALI

Asali ina virutubisho lukuki vinavyoifanya iwe ni chakula bora na dawa madhubuti ya kutibu magonjwa mengi. Kutokana na kuwa na kiasi kikubwa sana cha sukari. (high sugar concentration) kikaribiacho 80%( huku 20% iliyobaki ni maji)  huifanya asali iwe na tabia ya kuua vimelea (antibiotic properties) na kuzuia vimelea kuzaliana na kukua. Asali pia ina vimeng'enyo ( enzymes) ambavyo hutengeneza kemikali iitwayo Hydrogen peroxide (H202) , kemikali hii ina uwezo wa kuua bacteria wengi kwa wigo mkubwa (kills bacteria in abroad spectrum) na pia asali ina tindikali nyingi (highly acidic) kuiwezesha pia kuua vimelea. Asali ina vitamini na madini mbali mbali yanayoifanya iwe ni moja ya vyakula bora Duniani.

Source FANO 2010 products

No comments:

Post a Comment