Friday, July 12, 2013

FAIDA ZA ASALI

Sukari iliyoko kwenye asali humengenyuka kwa urahisi sana, na kugeuka kuwa glukosi na fruktosi kwa haraka. Hata kwa wale wenye matumbo mabovu (yenye maradhi).
Asali husaidia pia figo na utumbo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Asali ina kalories chache sana, ukilinganisha na kiwango cha sukari kilichomo kwenye asali, cha ajabu ni kuwa hutoa nishati (energy) nyingi katika mwili, lakini haisababishi ongezeko la mwili yaani unene. (Cholesterol)

Asali huyeyuka kwa haraka sana kuingia kwenye damu, ukilinganisha na vinywaji vingine, kama maji ya kawaida.  Asali huchukua takriban dakika saba tu kuingia katika mfumo wa damu.
Asali husaidia hutengenezaji wa damu mwilini, kwani hutoa nishati au nguvu inayosababisha hutengenezaji wa damu kuwa rahisi. Vilevile asali usafisha damu, katika mzunguko wake, na kusaidia mzunguko wa damu kuwa rahisi na mwepesi. Asali husadia kulinda mishipa ya damu isiathirike na maradhi yanayoshambulia mishipa ya damu. Asali pia husaidia kulinda ubongo na kuuwezesha kufanya kazi vizuri na upesi zaidi. Asali husaidia kuua bakteria wa aina mbalimbali inapotumiwa kwa matibabu na hasa kwenye vidonda. Pia asali husaidia kuondoa matatizo ya tishu (Tisue Difficiency) na udhaifu kwenye mwili (Body Frailty).

4 comments:

  1. Nimefurahi kujifunza amanegi kuhusu matumizi ya asali. Ingekuwa vyema zaidi kama ungetuelekeza vipimo vya matumizi kwa kila ugonjwa. Asali yako ungeuza sana!

    ReplyDelete
  2. MKUU, UKO VIZURI, MIMI HUWANATUMIA ASALI MBICHI MARA MBILI KWA MWAKA KAMA KINGA NA AFYA YA MWILI MPAKA SASA NINAMIAKA 7 SIJAUGUA MALARIA

    ReplyDelete
  3. Nimejifunza asante ila asali ya nyuki wadogo in nzuri kuliko nyuki wakubwa? Na he ktk biashara in wepi wazuri kufuga?

    ReplyDelete
  4. Ahsante Sana kwa elimu nzuri kweli hapa nilipo ninayo asali wanyuki wadogo naipenda Sana

    ReplyDelete