Wadau wote karibuni sana kwenye maonyesho ya wakulima ya nane nane na kupita kwenye banda la SUA ambapo mtajipatia asali safi na halisi toka HONEY SPRING.
Karibuni wote na mwambie na mwenzio aje apate mambo mazuri
HONEY SPRING
This blog is devoted to give out different information concerning honey like different types of honey, their uses, how to differentiate real honey from fake ones and many other things. Come, educate yourself and place your order of good quality honey from honey spring.
Thursday, August 1, 2013
NANE NANE MOROGORO
Monday, July 22, 2013
ASALI NA KUTIBU MICHUBUKO AU VIDONDA
Asali imekua ikitumika katika kutibu michubuko au vidoka toka zamani na ilitumika zaidi katika kutibu vidonda vya wanajesgi katika vita vya dunia!
Asali ina tabia za "kianti-bacteria" kwasababu ya gesi ya HYROGEN PEROXIDE inayopatikana na hivyo kufanya iwe na uwezo wa kupambana na bacteria lakini pia kuzuia mazingira ya bacteria kuzaliana!
Kutokana na sababu hizo ni vyema kutokosa asali katika sehemu tunazokaa ili kuweza kua na uhakika wa kujiponya wenyewe kwa haraka zaidi bila kuhangaika!
Pichani anaonekana mtoto mwenye michubuko ikiwa imepakwa asali ambayo ilikausha michubuko hiyo baada ya siku chache
Wednesday, July 17, 2013
ASALI TOKA HONEY SPRING
Honey Spring tuna ujazo tofauti wa asali kuanzia lita 5 hadi 350ml tukilenga kufikia watu wote ili kuongeza matumizi ya asali katika jamii zetu.
ASALI YA NYUKI WAKUBWA ambayo kwetu sisi inaitwa WAKUBWA CLASSIC ina ujazo(ikiwa na bei kwenye mabano) wa LITA 5(60, 000), LITA 1(12, 000) na 350ml(5500)
ASALI YA NYUKI WADOGO ambayo kwetu sisi inaitwa WADOGO CLASSIC ina ujazo(ikiwa na bei kwenye mabano) wa LITA 5(175, 000), LITA 1(35, 000), NUSU LITA(20, 000) na 350ml(15, 000).
Ukiwa unahitaji asali toka kwetu na upo DAR ES SALAAM unaweza piga simu namba 0683370065 au 0769129351 na ukatoa order yako na ukaletewa asali ulipo.
Kwa wakazi wa MOROGORO karibuni sana katika duka pekee la asali mkoani morogoro lililopo katika ghorofa la LOTTOS.
Tuesday, July 16, 2013
HONEY
Not All Sugars are Equal
The reasoning here is not about eating excessively and a willful binging of sugary stuff, which is all straight-forward enough for us to leave that stone unturned. I am talking about choosing honey over other sugars and eating it for health. Knowledge such as "there are good calories and bad calories" and "not all fats are equal" all seem too common, especially amongst people who are dieting and weight conscious, however "all sugars are not created equal" sometimes seems to come across as counter intuitive and even bizarre. People need to know that there are good sugar, bad sugar and even dangerous sugar! And because there are so many guises of sweeteners, and some come in names that you can even pronounce, we must know how to read food labels critically!
Think about it. Which sugar amongst all sugars fits this behavior - it is anabolic, medicinal, antiseptic, anti-cancer, gentle on blood sugar, friendliest to our liver, the most ideal fuel for burning body fats, and has many healing effects? None, except honey. Taste aside (though I vote it as the tastiest sugar, sweetest medicine), I believe bee's sugar is the best, nature-given sugar for our body, yet probably most forgotten and neglected sweetener. The doctors never fail to tell us that our body is unable to utilize refined sugars which are void of all nutrients and our body tissues in fact must relinquish precious vitamins and minerals to detoxify and eliminate them from our system, which often leads to nutrient deficiencies and the gradual deterioration of our cells and organs. But did they ever tell you once that our body needs some sugar, and good sugar, honey ideally, can provide a positive supply of liver glycogen for healthy effects of brain metabolism?
Friday, July 12, 2013
FAIDA ZA ASALI
Sukari iliyoko kwenye asali humengenyuka kwa urahisi sana, na kugeuka kuwa glukosi na fruktosi kwa haraka. Hata kwa wale wenye matumbo mabovu (yenye maradhi).
Asali husaidia pia figo na utumbo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa.
Asali ina kalories chache sana, ukilinganisha na kiwango cha sukari kilichomo kwenye asali, cha ajabu ni kuwa hutoa nishati (energy) nyingi katika mwili, lakini haisababishi ongezeko la mwili yaani unene. (Cholesterol)
Asali huyeyuka kwa haraka sana kuingia kwenye damu, ukilinganisha na vinywaji vingine, kama maji ya kawaida. Asali huchukua takriban dakika saba tu kuingia katika mfumo wa damu.
Asali husaidia hutengenezaji wa damu mwilini, kwani hutoa nishati au nguvu inayosababisha hutengenezaji wa damu kuwa rahisi. Vilevile asali usafisha damu, katika mzunguko wake, na kusaidia mzunguko wa damu kuwa rahisi na mwepesi. Asali husadia kulinda mishipa ya damu isiathirike na maradhi yanayoshambulia mishipa ya damu. Asali pia husaidia kulinda ubongo na kuuwezesha kufanya kazi vizuri na upesi zaidi. Asali husaidia kuua bakteria wa aina mbalimbali inapotumiwa kwa matibabu na hasa kwenye vidonda. Pia asali husaidia kuondoa matatizo ya tishu (Tisue Difficiency) na udhaifu kwenye mwili (Body Frailty).
MANUFAA YA ASALI
Zaidi ya kuwa tu chakula kinachofaa, asali ni mojawapo ya dawa za zamani zaidi zinazotumika, kwani ina vitamini B nyingi, madini kadhaa, na vitu vyenye uwezo wa kuzuia utendaji wa oksijeni. Dakt. May Berenbaum, mtaalamu wa wadudu katika Chuo Kikuu cha Illinois, Marekani, anasema: “Asali imetumiwa kwa karne nyingi kutibu matatizo mengi ya afya kama vile vidonda, kuungua, watoto wa jicho, vidonda vya ngozi na majeraha ya kukwaruzwa.”
Likieleza kuhusu upendezi wa hivi karibuni kuhusu manufaa za asali kwa afya, Shirika la Habari la CNN linaripoti hivi: “Asali iliacha kupakwa kwenye vidonda wakati dawa za kuua viini vya ugonjwa zilipovumbuliwa wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu. Lakini utafiti mpya na kutokea kwa bakteria zisizoweza kuuawa na dawa hizo umefanya asali ianze kutumiwa tena.” Kwa mfano, sehemu moja ya utafiti huo inahusu kutibu majeraha ya kuungua. Ilionekana kwamba wagonjwa walipona haraka na kuhisi maumivu machache na kuwa na makovu machache walipotibiwa kwa asali.
Uchunguzi unaonyesha kwamba kwa sababu ya kimeng’enya fulani kinachoongezwa kwenye nekta na nyuki, asali ina uwezo wa kupigana na bakteria na viini. Kimeng’enya hicho hutokeza haidrojeni peroksaidi, ambayo huua bakteria hatari. Isitoshe, inapopakwa juu ya kidonda, asali hupunguza mwasho na kuchochea ukuzi wa tishu zinazofaa. Hivyo, mtaalamu wa biolojia na kemia Dakt. Peter Molan wa New Zealand anasema: “Wataalamu wa matibabu wanaiona asali kuwa dawa nzuri, inayofaa kwa matibabu.” Kwa kweli, Shirika la Matibabu la Australia limeidhinisha asali kuwa dawa, na asali huuzwa kama dawa ya kutibu vidonda katika nchi hiyo.
Ni vyakula gani vingine vitamu ambavyo hujenga mwili na vinavyoweza kutumiwa kama dawa? Si ajabu kwamba zamani sheria zilipitishwa ili kulinda nyuki na wafugaji wa nyuki! Ilikuwa kosa kukata miti au kuharibu mizinga yenye nyuki, na mtu angeweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini kubwa au hata kuuawa
Thursday, July 11, 2013
ASALI NI NINI?
Sasa basi Asali ni nini? Asali ni mchanganyiko wa virutubisho mbali mbali, zikiwemo aina ya sukari zinazojulikana kwa jina la Glukosi (Glucose) pamoja na Fruktosi (Fructose), na madini mbalimbali vikiwemo; Magnesium, Copper, Iodine, zinc, Potassium, Calcium, Sodium, Chlorine, Sulfur, Iron na Phosphate, pamoja na vitamin B1, B2, B3, B5, B6, na vitamin C. Vitamin mara nyingi ubadilika kulingana na ubora wa necta, pamoja na chavua. Vile vile kwenye asali, kunapatikana aina mbalimbali za Hormones. Kama inavyoelezwa kuwa asali ni ponyo(kinywaji chenye kutibu) kwa wanadamu, na haya yamethibiti kwa wanadamu hivi leo. Kama ilivyotokea katika mkutano wa wanasayansi, uliofanyika mwaka 1993 mwezi Sept. tarehe 20-26. Mkutano huu ulifanyika nchini China, na ulijulikana kwa jina la World Apiculture Comference. Na kuchapishwa katika jarida la Horriget News Paper, la tarehe 19th.Oct.1993. Katika mkutano huo matibabu ya kutumia asali yalijadiliwa kwa mapana sana, wanasayansi wa Kimarekani wao walielezea kuwa, ndani ya asali kuna vitu vinaitwa; Royal Jelly, chavua, na ute (Propolis, Bee resin), vitu hivi husaidia sana katika matibabu ya magonjwa mengi. Naye Daktari kutoka Romania, yeye aliwahi kujaribu kutibu mtoto wa jicho (Cataract), kwa wagonjwa 2094, kati yao 2002 walipona kabisa, na hii ni sawa na asilimia 96% ya wagonjwa waliopona kabisa. Daktari huyo alieleza kuwa Bee Resin au ute unaotokana na nyuki, unasaidia kuponyesha magonjwa mengine, mfano magonjwa ya ngozi (Skin Diseases), magonjwa ya kuvuja kwa damu (Haemorrhoid), magonjwa ya uzazi (Gynaecological Diseases) n.k.