Sunday, June 30, 2013

UTATOFAUTISHAJE ASALI YA NYUKI WAKUBWA NA WADOGO?

Kama tujuavyo kua kuna aina mbili za asali ambazo ni ASALI YA NYUKI WAKUBWA na ASALI YA NYUKI WADOGO. Swali ni je mtu utatofautishaje kwa urahisi asali hizi na kuepuka kuibiwa na wajanja kabla ya kununua!!
Njia rahisi kabisa ya kutofautisha ni kwa kuonja asali hizo kwani zina LADHA tofauti.
ASALI YA NYUKI wadogo ina ladha ya UCHACHU inapomalizikia mdomoni wakati
ASALI YA NYUKI WAKUBWA yenyewe in a ladha ya UTAMU moja kwa moja bila kuacha uchachu mdomoni.

Njia nyingine ya kutofautisha kati ya asali hizi ni kua ASALI YA NYUKI WADOGO ni nyepesi zaidi kwasababu ina kiwango kikubwa zaidi cha maji kuliko ASALI YA NYUKI WAKUBWA ambayo ina kiwango kidogo cha maji na hivyo kuifanya iwe nzito zaidi.

TAHADHARI: Asali tunazozungumzia hapa ni zile ambazo ni HALISI na sio zilizochakachuliwa kwa njia yoyote.

AINA MBILI ZA ASALI NI...

Kuna aina kuu mbili za ASALI ambazo ndizo zinazojulikana ulimwenguni kote!
Aina hizo ni ASALI YA NYUKI WADOGO ( au asali ya nyuki wasiouma) na ASALI YA NYUKI WAKUBWA ( au asali ya nyuki wanaouma).
Aina hizo kuu mbili za nyuki ndizo zinatoa aina mbili kuu za asali!
Hivyo jambo la muhimu kujua kabla ya kununua asali ni kua kuna aina mbili za asali na hivyo ni lazma ujue unahitaji asali ipi, eidha ya NYUKI WAKUBWA au NYUKI WADOGO!
Ntakuja kueleza utofauti uliopo na jinsi gani ya kugundua utofauti uliopo kati ya aina hizo mbili za asali!

Usiache kufuatilia..

Picha inamuonyesha kushoto nyuki mkubwa anaeuma na kulia nyuki mdogo asieuma.