Zaidi ya kuwa tu chakula kinachofaa, asali ni mojawapo ya dawa za zamani zaidi zinazotumika, kwani ina vitamini B nyingi, madini kadhaa, na vitu vyenye uwezo wa kuzuia utendaji wa oksijeni. Dakt. May Berenbaum, mtaalamu wa wadudu katika Chuo Kikuu cha Illinois, Marekani, anasema: “Asali imetumiwa kwa karne nyingi kutibu matatizo mengi ya afya kama vile vidonda, kuungua, watoto wa jicho, vidonda vya ngozi na majeraha ya kukwaruzwa.”
Likieleza kuhusu upendezi wa hivi karibuni kuhusu manufaa za asali kwa afya, Shirika la Habari la CNN linaripoti hivi: “Asali iliacha kupakwa kwenye vidonda wakati dawa za kuua viini vya ugonjwa zilipovumbuliwa wakati wa Vita vya Pili vya Ulimwengu. Lakini utafiti mpya na kutokea kwa bakteria zisizoweza kuuawa na dawa hizo umefanya asali ianze kutumiwa tena.” Kwa mfano, sehemu moja ya utafiti huo inahusu kutibu majeraha ya kuungua. Ilionekana kwamba wagonjwa walipona haraka na kuhisi maumivu machache na kuwa na makovu machache walipotibiwa kwa asali.
Uchunguzi unaonyesha kwamba kwa sababu ya kimeng’enya fulani kinachoongezwa kwenye nekta na nyuki, asali ina uwezo wa kupigana na bakteria na viini. Kimeng’enya hicho hutokeza haidrojeni peroksaidi, ambayo huua bakteria hatari. Isitoshe, inapopakwa juu ya kidonda, asali hupunguza mwasho na kuchochea ukuzi wa tishu zinazofaa. Hivyo, mtaalamu wa biolojia na kemia Dakt. Peter Molan wa New Zealand anasema: “Wataalamu wa matibabu wanaiona asali kuwa dawa nzuri, inayofaa kwa matibabu.” Kwa kweli, Shirika la Matibabu la Australia limeidhinisha asali kuwa dawa, na asali huuzwa kama dawa ya kutibu vidonda katika nchi hiyo.
Ni vyakula gani vingine vitamu ambavyo hujenga mwili na vinavyoweza kutumiwa kama dawa? Si ajabu kwamba zamani sheria zilipitishwa ili kulinda nyuki na wafugaji wa nyuki! Ilikuwa kosa kukata miti au kuharibu mizinga yenye nyuki, na mtu angeweza kuadhibiwa kwa kutozwa faini kubwa au hata kuuawa
This blog is devoted to give out different information concerning honey like different types of honey, their uses, how to differentiate real honey from fake ones and many other things. Come, educate yourself and place your order of good quality honey from honey spring.
Friday, July 12, 2013
MANUFAA YA ASALI
Thursday, July 11, 2013
ASALI NI NINI?
Sasa basi Asali ni nini? Asali ni mchanganyiko wa virutubisho mbali mbali, zikiwemo aina ya sukari zinazojulikana kwa jina la Glukosi (Glucose) pamoja na Fruktosi (Fructose), na madini mbalimbali vikiwemo; Magnesium, Copper, Iodine, zinc, Potassium, Calcium, Sodium, Chlorine, Sulfur, Iron na Phosphate, pamoja na vitamin B1, B2, B3, B5, B6, na vitamin C. Vitamin mara nyingi ubadilika kulingana na ubora wa necta, pamoja na chavua. Vile vile kwenye asali, kunapatikana aina mbalimbali za Hormones. Kama inavyoelezwa kuwa asali ni ponyo(kinywaji chenye kutibu) kwa wanadamu, na haya yamethibiti kwa wanadamu hivi leo. Kama ilivyotokea katika mkutano wa wanasayansi, uliofanyika mwaka 1993 mwezi Sept. tarehe 20-26. Mkutano huu ulifanyika nchini China, na ulijulikana kwa jina la World Apiculture Comference. Na kuchapishwa katika jarida la Horriget News Paper, la tarehe 19th.Oct.1993. Katika mkutano huo matibabu ya kutumia asali yalijadiliwa kwa mapana sana, wanasayansi wa Kimarekani wao walielezea kuwa, ndani ya asali kuna vitu vinaitwa; Royal Jelly, chavua, na ute (Propolis, Bee resin), vitu hivi husaidia sana katika matibabu ya magonjwa mengi. Naye Daktari kutoka Romania, yeye aliwahi kujaribu kutibu mtoto wa jicho (Cataract), kwa wagonjwa 2094, kati yao 2002 walipona kabisa, na hii ni sawa na asilimia 96% ya wagonjwa waliopona kabisa. Daktari huyo alieleza kuwa Bee Resin au ute unaotokana na nyuki, unasaidia kuponyesha magonjwa mengine, mfano magonjwa ya ngozi (Skin Diseases), magonjwa ya kuvuja kwa damu (Haemorrhoid), magonjwa ya uzazi (Gynaecological Diseases) n.k.
HONEY AND BURNS
This is why it is recommended to have at least a small amount of honey at any time in our homes because accidents occur without warning!
Follow the instructions on the picture and you will be oky.
Wednesday, July 10, 2013
STINGLESS BEES HONEY vs STINGING BEES HONEY
How can I tell the difference between honey bee honey and stingless bee honey?
Stingless bee honey is more liquid than the well known honey bee honey. Honey bee honey has a water content of about 20% while the stingless bees has a water content of between 20-42%, depending on the species and the area from where the honey is collected. The high water content in stingless bee honey makes it very prone to fermentation. The flavor is often described as a more flowery than honey bee honey, but it depends largely on the species. There has been relatively little scientific research into the medical properties attributed to honey from stingless bees, but due to the presumption that it is a remedy and the usually low amount of honey produced, the price is much higher than that of honey bee honey (Apis mellifera).
IJUE ASALI ZAIDI
VIRUTUBISHO VILIVYOPO NDANI YA ASALI
Asali ina virutubisho lukuki vinavyoifanya iwe ni chakula bora na dawa madhubuti ya kutibu magonjwa mengi. Kutokana na kuwa na kiasi kikubwa sana cha sukari. (high sugar concentration) kikaribiacho 80%( huku 20% iliyobaki ni maji) huifanya asali iwe na tabia ya kuua vimelea (antibiotic properties) na kuzuia vimelea kuzaliana na kukua. Asali pia ina vimeng'enyo ( enzymes) ambavyo hutengeneza kemikali iitwayo Hydrogen peroxide (H202) , kemikali hii ina uwezo wa kuua bacteria wengi kwa wigo mkubwa (kills bacteria in abroad spectrum) na pia asali ina tindikali nyingi (highly acidic) kuiwezesha pia kuua vimelea. Asali ina vitamini na madini mbali mbali yanayoifanya iwe ni moja ya vyakula bora Duniani.
Source FANO 2010 products
MAFUNZO KUTOKA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII
Wizara ya Maliasili na Utalii imewafunza wananchi
namna ya kubaini Asali isiyokuwa halisi ambayo
inadaiwa kutengezwa na wafanyabishara kwa
kutumia maji ya miwa yaliyochemshwa na
kubadilika kuwa sukari guru.
Akizungumza NIPASHE katika maonyesho ya
biashara ya 37 yanayoendelea katika viwanja vya Mwalimu Nyerere Jijini Dar e
Salaam jana, Ofisa nyuki na wakala wa huduma za misitu kutoka wizara hiyo,
Theresia Kamote, alisema kuna njia kadhaa za kuitambua asali iliyochakachuliwa.
Kamote alizitaja njia hizo kuwa ni pamoja na kuweka maji kwenye glasi na kisha
kumimina Asali na kwamba ikikaa chini ya glasi bila kuchanganyana na maji basi hiyo ni asilia na inakuwa haijachanganywa na chochote.
Alisema njia ya pili ni kuiweka Asali kwenye njiti ya kibiriti na kisha kuiwasha ikiwa
njiti hiyo itawaka basi Asali haijachakachuliwa kwa kuchanganywa na chochote lakini njiti ya kiberiti isipowaka inakuwa ni feki.
Aidha, Kamote aliongeza kuwa wizara yake imekuwa ikiwasisitiza wafanyabiashara
wa bidhaa hiyo kuwa waaminifu na kuwauzia wateja waoe bidhaa halisi na wale ambao bidhaa zao zinagundulika zimechakachuliwa ziharibiwa.
Aliongeza kuwa njia nyingine ni kuonja bidhaa hiyo na kwamba iliyokachuliwa kwa
kuchemsha inatoa harufu ya moshi tofauti na ambayo ni halisi.
“Wizara imekuwa ikitoa rai kwa wafanyabiashara wa bidhaa hiyo kuwa waaminifu na
pale tunapogundua bidhaa yenyewe ni feki sisi kama wizara huwa tunaiharibu,”
alisisitiza Kamote.
Friday, July 5, 2013
KUOKA KWA KUTUMIA ASALI
Kwenye picha ni vitu vya kuzingatia ukiwa unatumia ASALI badala ya sukari katika kuoka vitu mbalimbali!
Tuanze kutumia asali sasa