Friday, July 5, 2013

ASALI na MDALASINI

Mchanganyiko huu ni tiba kubwa sana ambayo imekua ikishauriwa na matabibu kote duniani na bado tafiti mbali mbali zinaendelea kufanyika kuhusu mchanganyiko huu!
Tusiache afya zetu zidorore wakati dawa tunazo majumbani

Wednesday, July 3, 2013

MAJI KWENYE ASALI

Katika vitu ambavyo ni changamoto kubwa sana katika soko la asali na vinawasumbua si tu watumiaji wa asali bali hata wa wauzaji ni kiwango kikubwa cha maji katika asali kuliko kawaida ambacho chanzo huweza kua UWAHISHAJI WA KUVUNA ASALI KABLA HAIJAKOMAA VIZURI au tatizo kubwa zaidi ambalo ni UCHAKACHUAJI WA ASALI KWA KUONGEZA MAJI unaofanywa na wauzaji wasio waaminifu.

Kwa kawaida ASALI YA NYUKI WAKUBWA inakua na kiwango cha maji ya kati ya asilimia 17 mpaka 20 na asilimia inayobaki ni SUKARI. Wakati asali ya nyuki wadogo kiwango cha maji kinakua zaidi ya asilimia 20.

MAJI ni adui mkubwa sana katika asali kwani maji yakizidi hupunguza ubora wa asali, lakini pia huiweka asali katika hatari kubwa ya kuchacha.

Zipo njia nyingi za kienyeji za kupima kiwango cha maji kwenye asali na kujua kama maji yaliyopo ni ya kiwango sahihi ama la! Njia hizo ni pamoja na kutumia MSHUMAA, KARATASI NYEUPE, KUDONDOSHEA ASALI KWENYE KIKOMBE CHA MAJI n.k.

Pamoja na uwepo wa njia hizo lakini honey spring tumekwenda hatua moja mbele na tunatumia kifaa kidogo cha mkononi kinachoitwa REFRACTOMETER ambacho hupima kwa usahihi zaidi kiwango cha MAJI na SUKARI pia katika asali.

Kifaa hichi kinatuwezesha kuingiza sokoni asali ambayo inatakiwa kupelekwa kwa mlaji lakini pia kwa kiwango ambacho mlaji anakitegemea kwenye asali anayonunua!

Kwenye maonyesho ya nane nane(88) mwaka huu mkoani MOROGORO tutakuepo na kuonyesha vizuri zaidi watumiaji jinsi kifaa hichi kinavyofanya kazi.

Tuesday, July 2, 2013

ASALI NA RANGI ZAKE

Asali duniani kote haina rangi moja maalumu, ni muhimu sana kujua hilo!
Asali hutofautiana rangi kutokana na aina ya maua ambayo nyuki wanachukua nectar zao lakini pia kutokana na asali imekaa mda gano toka ilipovunwa na kuhifadhiwa!
Hautakiwi kustuka unapokutana na rangi tofauti ya asali kuliko ile uliyoizoea, mfano wa rangi za asali ni kama zinavyoonekana asali za rangi tofauti tofauti kwenyw picha!!

VITU VYA MOTO HAPANA

nawakaumbusha mnapotumia ASALI usiweke kwenye maji ya moto au chai ya moto sana kwasababu kwa kufanya hvyo utaua enzymes(vimeng'enyo) vyenye manufaa katika mwili!!
Asali ichanganywe kwenye maji au chai ya uvuguvugu ili kutoharibu uhalisia wake!!

MCHANGANYIKO WA ASALI NA MDALASNI

Anza siku yako kwa kunywa mchanganyiko wa ASALI na MDALASINI kwenye maji ya uvuguvugu kwenye uwiano wa angalau vijiko viwili vya asali kwa kimoja cha mdalasini. Mchanganyiko huu husaidia mambo mengi mwilini ikiwemo kusafisha kibofu cha mkojo, kusafisha tumbo, kuupa mwili nguvu, kupunguza cholestrol mwilini, kuponya kifua na mengine mengi. Anza sasa kwa maana ni kwa afya yako na usisubiri mpaka ushauriwe na daktari.

Asubuhi njema

Monday, July 1, 2013

KUTAMBUA ASALI HALISI

Kutokana na udanganyifu ambao watu wamekua wakifanya kwa kuchanganya asali na maji, sukari na vitu vingine ambavyo sio asali ni muhimu kujua njia za kutambua uhakisia wa asali!!

Njia mojawapo ni ya kutumia MSHUMAA katika kutambua uhalisia wa asali!
Chukua mshumaa na kisha chovya utambi wake katika asali kisha washa moto utambi. Endapo utambi utawaka basi asali hiyo ni halisi kwa maana ikiwa imechanganywa na kitu ambacho sio asali utambi hautaweza kuwaka.

Fata step kama inavyoonekana kwenye picha.

HOW TO DISTINGUISH REAL FROM FAKE HONEY

Save this for your future use and avoid being tricked!!